• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA:Kivumbi kuruka Jumamosi, baina ya watani wa jadi Simba na Yanga wakichezeshwa na refa mwanamke

  (GMT+08:00) 2020-01-02 08:42:26

  Ikiwa ule mtanange wa watani wa jadi ukisubiriwa kwa hamu Jumamosi hii ya tarehe 4, nchini Tanzania refa wa kike, Jeonesia Rukyaa atachezesha mechi hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya Simba SC na Yanga itakayotimua vumbi kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Jeonesia mwenye uzoefu sasa wa kuchezesha mechi hizo, Jumamosi atasaidiwa na washika vibendera Soud Lila na Hamisi Chang'walu wote wa Dar es Salaam. Refa wa akiba atakuwa Heri Sasii wa Dar es Salaam, Kamishna Khalid Bitebo 'Zembwela' kutoka Mwanza na Mtathmini Mchezo, Soud Abdi wa Arusha. Katika mechi mbili za msimu uliopita baina ya wababe hao wa soka ya Tanzania, ya kwanza ilimalizika kwa sare ya 0-0 Septemba 30, mwaka 2018 na ya pili Simba SC ikashinda 1-0 bao pekee la Meddie Kagere dakika ya 72 Februari 16, mwaka 2019 msimu ambao Wekundu wa Msimbazi waliibuka tena mabingwa wa Ligi Kuu. Simba SC ndiyo inayongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 34 baada ya kucheza mechi 13, ikiwazidi pointi 10 mahasimu wao hao wa jadi, Yanga SC ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako