• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TUZO: Kombora la Victor Wanyama katika tuzo ya bao bora

  (GMT+08:00) 2020-01-02 08:43:24

  Huku Victor Wanyama akizidi kuhusishwa na tetesi za kuondoka klabu yake ya Tottenham Hotspur katika kipindi kifupi cha uhamisho kilichoanza jana Jumatano, kombora la nahodha huyo wa timu ya taifa ya Kenya dhidi ya Liverpool msimu uliopita linawania bao la mwongo. Katika tovuti ya klabu hiyo ya jijini London, Uingereza, bao hilo la Wanyama limetiwa kwenye orodha ya mabao 25 yaliyofungwa kati ya mwaka 2010 na 2019 yanayowania tuzo hiyo. Wanyama, ambaye tetesi zimekuwa zikisema anamezewa mate na Hertha Berlin (Ujerumani), Celtic (Scotland) na klabu za hapa China, aliingia mechi ya Liverpool kama mchezaji wa akiba zikisalia dakika 10 mchuano huo utamatike mnamo Februari 4, 2018. Dakika mbili tu baada ya kujaza nafasi ya Mbelgiji Mousa Dembele, Wanyama alivuta kiki nzito kutoka nje ya kisanduku akaibwaga wavuni, na kufanya mabao kuwa 1-1 katika mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). Alipiga shuti kali kutoka mita 27 ambalo Karius aliona likiwa ndani ya nyavu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako