• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwanariadha Gulam apelekwa Japan kusaka viwango vya Olimpiki

  (GMT+08:00) 2020-01-02 16:18:10

  Shirikisho la RIadha Tanzania (RT) limepanga kumpeleka kambini nchini Japan mwanariadha Ally Gulam kwa lengo la kujiandaa na michezo ya Olimpiki ya Tokyo itakayoanza Julai 24 hadi Agosti 9 mwaka huu nchini Japan. Nchi mbalimbali zitashiriki katika michezo hiyo ikiwemo Tanzania ambayo mpaka sasa wanariadha Alphonce Simbu na Failuna Abdi wamefikia viwango vya kushiriki. Shirikisho hilo linahitaji kuona idadi ya washiriki wa mashindano ya Olimpiki inaongezeka na kuwa na washiriki wa mbio ndefu na za kati.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako