• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilivunja rekodi kwa kukusanya asilimia 100.02 ya mapato yake yote mnamo Desemba 2019

  (GMT+08:00) 2020-01-02 19:40:06
  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilivunja rekodi kwa kukusanya asilimia 100.02 ya mapato yake yote mnamo Desemba 2019, ikizidi matarajio ya miezi.

  Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Edwin Mhede amesema kuwa TRA ilikusanya Sh1.987 trilioni kutoka kwa vyanzo mbali mbali vya mapato dhidi ya matarajio yake ya Sh1.983 trilioni .

  Ikilinganishwa na mwaka wa 2018, Dk Mhede amesema kiwango cha ukuaji wa makusanyo ni asilimia 22.05 kutoka Sh1.628 trilioni zilizokusanywa mnamo Desemba 2018.

  Mkusanyaji ushuru pia alikusanya Sh1.484 trilioni mwezi Oktoba na Sh1.501 trilioni mnamo Novemba 2019, sawa na asilimia 93.98 na asilimia 97.59 ya matarajio yao.

  Aidha amesema lengo lao ilikuwa ni kukusanya sh trilioni 1.579 na sh trilioni 1.538 mwezi oktoba na novemba mwaka 2019.

  Mafanikio haya mazuri, yalichangiwa na , utekelezaji wa sheria na kanuni zilizopo, kusimamia mianya ya ukwepaji kodi, elimu kwa walipa kodi, kusimamia utoaji wa risiti za Kielektroniki (EFD) na kuboresha huduma.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako