• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Michael Sarpong akamilisha uhamisho naa kuja kucheza kwenye klabu ya China

  (GMT+08:00) 2020-01-03 13:12:43

  Mshambuliaji wa Rayon Sports Michael Sarpong amekuwa mwanasoka ghali zaidi kusainiwa katika ligi kuu ya Rwanda baada ya kukamilisha hatua yake ya kuhamia kwenye timu ya daraja la pili ya China Changchun Yatai. Mshambuliaji huyo mzaliwa wa Ghana ambaye amesafiri jana kuja China, amesainiwa kwa ada ya dola za kimarekani $650,000, ambapo kati ya hizo $150,000 zimekwenda kwenye timu yake ya sasa ya Rayon. Akiongea kabla ya kuja China Sarpong amesema ni changamoto kubwa kwake kwani kuna tofauti kubwa kati ya pande mbili akimaanisha Rwanda na China, lakini amethibitisha kuwa ana uhakika kuwa atazoea haraka na kufanya kila awezalo kutoa mchango kwa ajili ya mafanikio ya klabu yake. Amesisitiza kuwa anataka kuwaonesha Wachina kuwa hawakufanya makosa kumchagua yeye.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako