• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zanzibar: Rais apongeza sekta ya kibinafsi

  (GMT+08:00) 2020-01-03 17:18:43
  Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, amesema sekta ya kibinafsi ikiwamo biashara, zimekuwa na mchango kubwa sana katika maendeleo ya mataifa mbalimbali duniani. Rais aliyasema hayo jana katika ufunguzi wa jengo jipya la Shule ya Sekondari ya Biashara iliyoko Mombasa mjini Zanzibar.

  Alisema mwaka wa 1980 Serikali ya Zanzibar iliondokana na mfumo wa kuhodhi biashara na badala yake kujikita katika usimamizi wa sera na sheria ili kutoa fursa kwa wadau wa sekta hiyo kufanya shughuli hizo kwa upana.

  Rais aliwapongeza na kuwatambua wafanyibiashara wakiwamo wale wanaofanya vyema shughuli zao kwa uadilifu na kurejesha faida kwa jamii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako