• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zanzibar: Rais Mstaafu Karume asema ongezeko la benki ni ishara ya ukuaji uchumi

  (GMT+08:00) 2020-01-03 17:19:06

  Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, amesema kuongezeka kwa matawi ya huduma kwa Benki ya Watu wa Zaznibar (PBZ) ni ishara nzuri ya kukua kwa uchumi Zanzibar. Karume aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza katika sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo la benki hiyo,huko Malindi Unguja, ikiwa ni shamrashamra ya kutimiza miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Rais huyo mstaafu aliongeza kwa kusema kwamba kuimarisha shughuli za kibenki kwa kutumia njia za kiteknolojia kutawarahisishaia wateja kupata huduma kwa haraka. Alisisitiza kuwa hatua ya serikali kujenga matawi mbalimbali ya huduma za kibenki , itasaidia kuepusha msongamano wa wateja na kuwarahisishia wateja kupata huduma zao kwa haraka na kwa wakati unaofaa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako