• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Gharama ya maisha yapanda

  (GMT+08:00) 2020-01-03 17:19:27
  Wakenya huenda wakakumbwa na hali ngumu ya maisha baada ya bei ya bidhaa ambazo hununuliwa mara kwa mara kutoka madukani na sokoni kupanda. Bei imepanda juu kwa mwezi wan ne mtawalia, huku uzito ukiwa mzito zaidi mwezi Desemba, ambao umekamilika siku chache zilizopita.

  Kulingana na data iliyotolewa jana na shirika la kitaifa la Takwimu fumuko wa bei ulipanda hadi asilimia 5.82 mwezi Desemba mwaka uliopita, kutoka asilimia 5.56 mwezi Novemba mwaka uo huo.

  Wakenya waliotumia pesa nyingi wakati wa sherehe za krismasi na mwaka mpya, watalazimika kujinyima zaidi haswa shule zinapofunguliwa juma lijalo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako