• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: TRA yavuna pakubwa

  (GMT+08:00) 2020-01-03 17:20:10
  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imevunja rekodi kwa kukusanya Sh trilioni 1.987 kwa Desemba 2019, ikiwa ni kiasi kikubwa kuwahi kukusanywa katika mwaka mpya wa Serikali ulioanza Julai 2019.

  Akizungumza na wanahabari Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa TRA, Dk. Edwin Mhede alisema ni kweli kwamba kitaalamu, miezi tofauti hailingani moja kwa moja, lakini kwa makusanyo hayo ya Sh trilioni 1.987 kwa Desemba 2019, TRA imevunja rekodi yake yenyewe iliyoiandika Septemba 2019.

  Alisema kwa ulinganifu wake pekee ni kuwa kama ilivyo Desemba 2019, Septemba 2019 nao ulikuwa mwezi wa rekodi, kwa kukusanya Sh trilioni 1.7, iliyokuwa ni sawa na asilimia 97.20 ya lengo la kukusanya Sh trilioni 1.817.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako