• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaiunga mkono Korea Kaskazini kuendelea kukuza uchumi, kuinua kiwango cha maisha ya wananchi

    (GMT+08:00) 2020-01-03 18:51:27

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang hapa Beijing amesema, China inaiunga mkono Korea Kaskazini kuendelea kukuza uchumi wake, kuinua kiwango cha maisha ya wananchi, na kuzidi kupata maendeleo mapya katika ujenzi wa ujamaa.

    Geng amesema hayo kufuatia taarifa iliyotolewa baada ya kufungwa kwa Mkutano mkuu wa tano wa kamati kuu ya awamu ya saba ya chama cha wafanyakazi cha Korea Kaskazini. Amesema, mkutano huo umejumuisha maendeleo yanayopatikana kwenye sekta mbalimbali hasa sekta ya uchumi nchini Korea Kaskazini, huku ukithibitisha mwelekeo wa malengo na juhudi za maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika siku za baadaye.

    Bw. Geng pia amesema, taarifa ya mkutano huo pia imetoa ujumbe muhimu kwa uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Marekani. China inazitaka nchi hizo mbili kurejesha mazungumzo haraka iwezekanavyo na kufikia makubaliano, kufanya juhudi za pamoja na kutimiza mawasiliano, ili kufanya juhudi halisi katika kumaliza mvutano uliopo na kuhimiza utatuzi wa kisiasa wa suala la Peninsula ya Korea kupata maendeleo mapya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako