• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gazeti la New York Times latoa habari zisizo za kweli kuhusu utoaji wa nafasi za ajira mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2020-01-03 19:12:26

    Gazeti la New York Times la Marekani limetoa makala moja, ikisema serikali ya mkoa wa Xinjiang "inawalazimisha" watu wa kabila la Wauygur kufanya kazi, madai ambayo hayana msingi wowote na kupotosha ukweli wa kazi ya kawaida ya serikali ya huko ya kuwasaidia watu maskini na kutoa nafasi za ajira.

    Vurugu na umaskini ni kama pande mbili za sarafu moja. Tukiangalia dunia, nchi na sehemu zinazokumbwa na ugaidi na mawazo yenye siasa kali pia uchumi wake ni dhaifu. Ndiyo maana kukuza uchumi, kuongeza nafasi za ajira, na kuondoa umaskini ni hatua muhimu katika kutokomeza ugaidi na kurejesha utulivu wa jamii, hayo ni makubaliano ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa.

    Kutokana na mazingira ya kiasili na muundo wa kiuchumi, mkoa wa Xinjiang, haswa sehemu ya kusini ya mkoa huo ambako wanaishi watu wa makabila madogo madogo, umekuwa nyuma kiuchumi kwa muda mrefu. Ili kuzuia athari mbaya kutokana na mawazo yenye siasa kali kwa mkoa huo, serikali ya huko ilitoa kipaumbele katika kazi ya kuongeza nafasi za ajira, kuwasaidia watu maskini, na kuboresha maisha ya wananchi, na kuhakikisha kila familia kuna mtu zaidi ya mmoja mwenye ajira. Katika miaka mitano iliyopita, watu milioni 23.1 wameondokana na umaskini, kiwango cha umaskini kimepungua kutoka asilimia 22.84 ya mwaka 2014 hadi asilimia 6.51.

    Lakini Gazeti la New York Times halikutaja hata kidogo hali ya kuboreshwa kwa maisha ya mkoa wa Xinjiang, badala yake ilipotosha habari ya ongezeka la kiwango cha upatikanaji wa ajira mkoani humo na kudai kuwa wananchi wa makabila madogomadogo wanapata ajira kwa kulazimishwa na serikali, hata kuiita hali hiyo kuwa ni "maafa". Mbali na hayo, makala hiyo haikumhoji ofisa yeyote wa serikali ya mkoa wa Xinjiang, na takwimu zilizonukuliwa kwenye makala hiyo hazijathibitishwa.

    Jambo lingine la kushangaza ni kuwa makala hiyo inasema watu wengi wa Kituo cha Ufundi Stadi cha mkoa wa Xinjiang wanatumwa kufanya kazi kwenye viwanda baada ya kupewa mafunzo. Lakini ukweli ni kwamba, lengo la kuanzisha kituo hicho mkoani Xinjiang ni kuunganisha mapambano dhidi ya ugaidi, na kuondoa mawazo yenye siasa kali pamoja na kuboresha maisha ya wananchi. Na masomo ya chuo hicho yanatolewa kwa kukidhi mahitaji ya viwanda vya huko, ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa nguo na viatu, vyakula, uundaji wa mitambo ya kielektroniki na biashara ya kielektroniki.

    Hivi karibuni, mwandishi wa habari wa Shirika kuu la Utangazaji la China CMG alikwenda mkoani Xinjiang na kugundua kuwa, wanafunzi wa chuo hicho wameweza kupata uwezo wa kujitegemea kupitia kutafuta ajira au kuanzisha biashara binafsi baada ya kumaliza masomo yao. Kwa mfano, msichana mwenye umri wa miaka 26 anayeitwa Rukiya Yakup alisema alishughulikia kazi ya mauzo ya nyumba baada ya kumaliza masomo yake, na mshahara wake kwa mwezi umefikia dola za kimarekani elfu 1150, ambacho ni kiasi kikubwa ikilinganishwa na kiwango cha mapato cha huko.

    Ukweli hauwezi kufunikwa. Bila ya kujali baadhi ya vyombo vya habari na wanasiasa wanavyoupaka matope mkoa wa Xinjiang, watu walioutembelea mkoa huo wanaweza kupata hitimisho lao kwa mtazamo wa haki. Mwaka 2020 umewadia, Mkoa wa Xinjiang utashirikiana na sehemu nyingine mbalimbali nchini China, kutimiza lengo la kuondokana na umaskini kwa pande zote na kupata ustawi na utulivu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako