• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ubalozi wa Marekani wawataka raia wa nchi hiyo kuondoka haraka Iraq

  (GMT+08:00) 2020-01-03 19:27:35

  Ubalozi wa Marekani nchini Iraq umetoa tahadhari kwa raia wake kuondoka mara moja nchini humo, ikiwa ni saa chache baada ya shambulizi la anga lililofanywa na Marekani kusababisha kifo cha Kamanda wa juu wa Iran, Qassem Soleimani na makamu mkuu wa kikosi cha Hashd Shaabi cha Iraq Abu Mahdi al-Muhandis.

  Taarifa iliyotolewa na ubalozi huo imesema, kutokana na mvutano mkubwa kati ya Iraq na eneo hilo, ubalozi unawataka raia wake kuondoka mara moja kwa ndege inapowezekana, na ikishindikana, kwenda katika nchi nyingine kwa njia ya barabara.

  Pia ubalozi huo umewataka raia wa Marekani kuchukua hatua muhimu kama vile kutokwenda Iraq na kuepuka kwenda kwenye ubalozi wa Marekani nchini Iraq.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako