• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi asisitiza uhifadhi wa mazingira ya bonde la Mto Manjano

    (GMT+08:00) 2020-01-04 18:39:17

    Rais Xi Jinping wa China jana alisisitiza kuwepo juhudi za kuongeza ulinzi wa mazingira na maendeleo ya hali ya juu ya bonde la Mto Manjano, pamoja na kuhimiza ujenzi wa mzunguko wa uchumi katika miji ya magharibi ya Chengdu na Chongqing.

    Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC, na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, amesema hayo katika mkutano wa sita wa kamati kuu wa mambo ya fedha na uchumi. Viongozi waandamizi Li Keqiang, Wang Huning na Han Zheng pia wamehudhuria mkutano huo. Kwenye taarifa iliyotolewa bada ya mkutano huo, inasema ili kuimarisha ulinzi wa mazingira na maendeleo ya hali ya juu ya bonde la Mto Manjano, mkutano umesisitiza uhifadhi wa mazingira, maendeleo yasiyo na uchafuzi na kurejesha uasili wa mazingira. Aidha utumiaji maji usio na maana lazima uzuiliwe na kuchukiliwa hatua za kuondoa uchafuzi wa maji, hewa na udongo.

    Aidha mkutano umetoa wito wa kuchukuliwa juhudi za kuboresha muundo wa viwanda huku urithi wa utamaduni wa Mto Manjano ukihifadhiwa na kukuzwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako