• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China azungumza na wenzake wa Russia na Iran

    (GMT+08:00) 2020-01-05 18:13:34

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana kwa nyakati tofauti alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na wenzake wa Iran Bw. Javad Zarif na wa Russia Bw. Sergei Lavrov.

    Alipozungumza na Bw. Zarif Bw. Wang amesema, kitendo hatari cha jeshi la Marekani kimekiuka kanuni ya kimsingi ya uhusiano wa kimataifa, na kitaongeza msukosuko wa hali ya kikanda. Ameongeza kuwa, China inapinga matumizi ya nguvu katika uhusiano wa kimataifa, na kuitaka Marekani itatue masuala kwa njia ya mazungumzo.

    Bw. Zarif amefafanua msimamo wa Iran kuhusu Marekani kumwua jenerali wake, na kusema kitendo hicho cha Marekani kitasababisha matokeo mabaya. Ameiomba China ifanye kazi muhimu ili kuzuia ongezeko la msukosuko wa kikanda.

    Alipozungumza na Bw. Lavrov Bw. Wang amesema China inafuatilia ongezeko la mgogoro kati ya Marekani na Iran, na kuzitaka pande husika zifuate katiba ya Umoja wa Mataifa na kanuni za uhusiano wa kimataifa. Ameongeza kuwa, zikiwa wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, China na Russia zinatakiwa kulinda kwa pamoja sheria za kimataifa na haki za kimataifa, na kufanya kazi madhubuti kukabiliana na hali ya Mashariki ya Kati.

    Naye Bw. Lavrov amesema msimamo wa Russia uko sawa na wa China, na kitendo cha Marekani ni haramu na kinapaswa kulaumiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako