• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Trump atishia kushambulia vituo 52 Iran kama ikijibu kufuatia kuuawa kwa kamanda wake

  (GMT+08:00) 2020-01-05 18:20:36

  Rais Donald Trump wa Marekani ameionya Iran kuwa Marekani imelenga vituo vyake 52 na itashambulia "haraka na kwa nguvu" kama itaishambulia Marekani au raslimali zake.

  Rais Trump amesema wamelenga shabaha 52 kuwakilisha mateka 52 waliotekwa na Iran katika miaka ya nyuma, baadhi ya shabaha hizo ni za hali ya juu na muhimu kwa Iran na utamaduni wa Iran

  Tishio la Bw. Trump limekuja baada ya shambulizi la ndege la Marekani kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Baghdad kumuua Meja Jenerali Qassem Suleiman, kamanda wa kikosi cha ulinzi wa mapinduzi ya kiislamu cha Iran al Quds.

  Miji mikubwa ya Marekani ikiwa ni pamoja na Washington, New York na Los Angeles iko kwenye tahadhari baada ya shambulizi, pamoja na kuwa hakuna tishio lolote halisi dhidi ya miji hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako