Taarifa iliyotolewa jana na Ikulu ya Ufaransa imesema, rais Emmanuel Macron siku hiyo alizungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Marekani Donald Trump kuhusu hali ya mvutano katika kanda ya Mashariki ya Kati.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kwenye mazungumzo hayo rais Macron amesema Ufaransa inapenda kushirikiana kwa pamoja na pande mbalimbali za kikanda na kimataifa ili kupunguza mvutano wa sasa katika kanda ya Mashariki ya Kati, na kwamba muungano wa kimataifa unatakiwa kuheshimu kikamilifu mamlaka ya Iraq na kuendelea kutoa kipaumbele katika kupambana na kundi la kigaidi la IS, ili kuhakikisha usalama wa Iraq na utulivu wa kanda nzima.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |