• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sanamu ya Zlatan Ibrahimovic sasa yaangushwa chini

  (GMT+08:00) 2020-01-06 10:42:36

  Sanamu la mshambuliaji wa klabu ya AC Milan Zlatan Ibrahimovic lililopo nje ya uwanja wa klabu yake ya zamani iliyomlea Malmo huko chini Sweden lakatwa hadi kuanguka chini. Sanamu hiyo, awali lilikatwa pua baada ya Ibrahimovic kuwekeza katika klabu pinzani mnamo mwezi Disemba. Uharibifu huo uligunduliwa saa 3.30 asubuhi jana Jumapili, na kulikuwa na maneno ya kejeli na matusi" Polisi waliweka uzio kuzunguka sanamu hiyo, ambayo ilizinduliwa mwezi Oktoba 2019, pia Nyumba ya Ibrahimovic huko Stockholm iliharibiwa, kwa kuandikwa maneno mengi kama "Yuda" kwa kupakwa rangi kwenye mlango wa mbele. Ibrahimovic amesaini tena AC Milan. Anatarajiwa kuanza kuitumika ligi ya Serie A leo Jumatatu wakati watawakaribisha Sampdoria

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako