• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Trump yaendelea kuwa imara dhidi ya Iran licha ya ukosoaji wa wabunge

    (GMT+08:00) 2020-01-06 17:08:52

    Serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani jana iliendelea kutetea nia yake ya kuizuia Iran kuchukua hatua za mashambulizi ya kujibu kwa kauli za vitisho, wakati wabunge wa Marekani wanamlaumu Rais Trump kwa kutoa habari kupitia mitandao ya kijamii kuipeleka nchi kwenye eneo la hatari.

    Rais Trump ameonya kuwa Marekani itaishambulia vikali Iran kama ikijibu shambulizi kwa kumshambulia mmarekani yeyote na mali zozote. Kwenye ujumbe wake Rais Trump amesema ujumbe anaotoa kwa njia ya mitandao ya kijamii inalenga kulifahamisha bunge la Marekani kuwa kama Iran ikimshambulia mmarekani yeyote au shabaha yoyote, basi Marekani itajibu kwa haraka na kuwa ukamilifu, na ikiwezekana kupita kiasi.

    Maneno ya Rais Trump yamekuja baada ya kitisho cha kujibu mashambulizi kutoka kwa kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, kutokana na kuuawa kwa mkuu wa kikosi cha Quds cha jeshi la Iran Meja Jenerali Qassem Soleimani.

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo ametetea hatua ya serikali ya Marekani kumuua Meja jenerali Soleiman pamoja na ujumbe anaotoa kupitia mitandao ya kijamii. Bw. Pompeo amesema taarifa za kijasusi zimeonesha kuwa, hatari ya kutochukua hatua dhidi ya Meja Jenerali Soleimani ilikuwa kubwa kuliko kuchukua hatua.

    Hatua ya Marekani dhidi ya Iran imezusha mvutano kwenye bunge la Marekani, ambapo wabunge wamesema unaipeleka Marekani kwenye eneo la hatari. Seneta wa Chama cha Democrat Chris Murphy amesema hatua ya rais Trump imesababisha bunge la Iraq kufukuza wanajeshi wa Marekani, na kusimamisha operesheni za jeshi la Marekani na NATO dhidi ya kundi la ISIS.

    Kufuatia hatua hiyo ya bunge la Iraq, Rais Trump ametishia kuwa atachukua hatua za kuweka vikwazo vikali dhidi ya Iraq. Waziri mkuu wa muda wa Iraq Bw. Adel Abduk Mahdi ameongea kwenye mkutano wa bunge akisema kuondoka kwa jeshi la Marekani nchini kutakuwa na manufaa kwa Iraq na Marekani, hasa kutokana na hali ya sasa. Rais Trump amesema kama Iraq ikiwafukuza wamarekani, wataondoka kwa njia mbaya, na kuweka vikwazo vikali hata kuliko vya Iran. Rais Trump amesema Marekani imejenga kituo cha jeshi la anga cha gharama za mabilioni ya dola nchini Iraq, na haitaondoka kama Marekani haitalipwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako