• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya mpito ya Sudan inakabiliwa na wakati mgumu wa kufufua uchumi.

  (GMT+08:00) 2020-01-06 20:42:39
  Serikali ya mpito ya Sudan inaangali jinsi itafufua uchumi uliodorora wakati inawalinda raia kutokana na mshtuko wa mfumko kupitia ruzuku.

  Khartoum ilipitisha bajeti ya baada ya mapinduzi ya nchi hiyo wiki iliyopita na upungufu wa dola bilioni 1.62.

  Na wakati maoni ya bajeti yanaonyesha matumizi ya ziada kwenye elimu na afya, viongozi wamekuwa wakijaribu kuangalia kile cha kufanya na ruzuku kwa bidhaa za msingi.

  Utawala wa rais wa zamani Omar al-Bashir uliendesha uchumi kwa ruzuku kwenye gesi, mafuta, dawa muhimu na ngano.

  Lakini serikali ya Waziri Mkuu Abdalla Hamdok inakabiliwa na mtihani wa kuendelea na mtindo huo wa rais wa zamani, au kurekebisha ruzuku hiyo au kuifuta kabisa.

  Wataalam wamesema Uchumi duni wa Sudan unaofadhiliwa na gharama kubwa ya maisha, kuzorota kwa sarafu na vikwazo hufanya iwe sio busara kuendelea na sera hiyo ambayo iliona serikali ikikusanya hadi dola bilioni 2.250 kila mwaka katika ruzuku ya mafuta na dola milioni 365 kwa ngano.

  Wakosoaji wamesema kweli ruzuku hiyo ilinufaisha matajiri ambao walifanya biashara zao wakati wakichangiwa na serikali na kuuza bidhaa kwa watu masikini kwa bei kubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako