• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya kikapu Tanzania kushiriki michuano ya kufuzu kombe la Afrika kwa wanaume Kenya

  (GMT+08:00) 2020-01-07 08:48:49

  Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) kupitia kwa Rais wake, Phares Magesa limesema kuwa Januari 14 hadi 18, 2020 timu ya taifa ya kikapu itashiriki mashindano ya kufuzu kucheza kombe la Afrika kwa wanaume, yatayofanyika Nairobi, Kenya. Makocha walioteuliwa na kamati ya utendaji kuiongoza timu hiyo ni Alfred Ngalaji ambaye atasaidiana na Ashraf Haroun na makocha hao wameteua wachezaji watakaounda timu ya Taifa, ndani yake wakiwemo wachezaji wanne walioshiriki michuano ya Sprite Bball Kings 2019 wakiwemo Baraka Sadick ambaye alishinda tuzo ya MVP. Wachezaji wote wanatarajiwa kuripoti kambini kuanzia leo kwaajili ya maandalizi na timu inatarajiwa kuondoka tarehe 12 Januari, 2020 kuelekea Nairobi, Kenya tayari kwa mashindano hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako