• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu mkuu wa UM atoa mwito pande mbalimbali zijizuie ili mvutano usije ukapamba moto

  (GMT+08:00) 2020-01-07 08:56:05

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana ametoa mwito kwa pande mbalimbali zijiuie ili mvutano wa sasa usije ukapamba moto zaidi.

  Bw. Guterres amesema mvutano wa sasa umefikia kiwango cha juu zaidi katika karne hii, ambapo msukosuko unazidi kuongezeka, na hali ya kutoenezwa silaha za nyuklia haina uhakikisho tena. Amesema anawasiliana na viongozi wa baadhi ya nchi, akizihimiza pande husika kujizuia, ili kuepusha kupamba moto kwa mvutano, na kurejesha mazungumzo na ushirikiano wa kimataifa.

  Pia amesema, jumuiya ya kimataifa inapaswa kukumbuka maumivu makubwa yaliyosababishwa na vita kwa binadamu wote, na kwamba kuepusha vita ni wajibu wetu wa pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako