• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa Iraq asisitiza umuhimu wa kushirikiana na Marekani juu ya kuondoa vikosi vya kigeni

  (GMT+08:00) 2020-01-07 09:23:35

  Waziri mkuu wa Iraq Bw. Adel Abdul Mahdi amemthibitishia balozi wa Marekani nchini Iraq Bw. Matthew Tueller kuwa ni muhimu kushirikiana kuhusu kuondoa vikosi vya kigeni kwa mujibu wa uamuzi wa bunge la Iraq.

  Ofisi ya waziri mkuu wa Iraq imetoa taarifa ikisema Bw. Abdul Mahdi jana alikutana na Bw. Tueller, na kujadili hali ya maendeleo ya sasa pamoja na msimamo wa serikali ya Iraq. Bw. Abdul Mahdi amesema uondoaji wa vikosi vya kigeni utaweka msingi imara wa uhusiano kati ya Iraq na Marekani. Taarifa hiyo imeongeza kuwa Iraq inafanya kila juhudi kuzuia kutokea kwa vita.

  Wakti huohuo, waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. Mark Esper amesema Marekani haijaamua kuondoa vikosi vyake kutoka Iraq.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako