• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mazishi ya Qassem Soleimani yafanyika mjini Tehran

  (GMT+08:00) 2020-01-07 09:31:55

  Mazishi ya kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Qassem Soleimani aliyeuawa mjini Baghdad katika shambulizi la anga la Marekani, yamefanyika jana mjini Tehran, na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei na rais Hassan Rouhani wa nchi hiyo.

  Vyombo vya habari vya Iran vimesema malaki ya watu wa Iran waliandamana kwenye mitaa ya Tehran kuuaga mwili wa Bw. Suleimani, wakiwa wamevaa mavazi meusi.

  Wakatu huo huo waziri Mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu amesema kuwa nchi yake haijashiriki katika shambulizi la Marekani lililomwua Bw. Soleimani, na kusema Israel haitaki kuwa sehemu ya mvutano unaopamba moto kati ya Iran na Marekani.

  Bw. Netanyahu amesema hayo kwenye mkutano maalum wa baraza la usalama la Israel uliofanyika kujadili athari za mauaji ya Bw. Soleimani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako