• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Malkia Strikers yaendeleza umwamba michuano ya kufuzu Olimpiki kwa kuifunga Botswana

    (GMT+08:00) 2020-01-07 10:33:22

    Timu ya taifa ya Kenya ya volleyball kwa upande wa wanawake imeendeleza ubabe wake kwa kuitoa makamasi Botswana kwa seti (25-17, 25-19, 25-18) kwenye mechi yao ya pili ya michuano ya voliboli ya kufuzu Olimpiki ya Tokyo inayoendelea katika uwanja wa ndani wa Palais polyvalent des sports (Paposy). Kufuatia ushindi huo Malkia Strikers wanaongoza kwenye msimamo kwa pointi sita na leo wanatarajiwa kuvaana na mahasimu wao wakubwa Cameroon. Cameroon jana ilicheza na Nigeria katika mechi ya pili. Kwa sasa Cameroon ina pointi tatu walizozipata kwenye ushindi wao wa 3-0 walipocheza na Botswana Jumapili, huku Misri, Nigeria na Botswana wakifuata nyuma. Mechi ya leo itakuwa ya kufa na kupona kwani Kenya haijawahi kuishinda Cameroon nyumbani, hata hivyo kocha wa Malkia Strikers Paul Bitok amesisitiza kuwa amedhamiria kuandika historia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako