• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Klabu za Premier League mbioni kuisaka saini ya Mbwana Samatta

  (GMT+08:00) 2020-01-07 10:33:50

  Klabu ya Norwich City na Brighton zinazo shiriki ligi kuu England zimeanza kumuulizia mshambuliaji hatari wa KRC Genk na timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta. Licha ya timu hizo kuingia katika vita vya kutafuta saini ya nyota huyo wa Kimataifa wa Tanzania inaelezwa thamani yake ni pauni milioni 10. Mbali na Norwich City na Brighton inadaiwa kuwa Samatta ambaye msimu huu tayari ameshatupia kambani jumla ya mabao 10 yakiwemo yale matatu kwenye michuano ya Champions League alipoifunga Liverpool na RB Salzburg lakini pia anawaniwa na timu ya Eintracht Frankfurt pamoja na Lazio. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 27, msimu uliyopita alikuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Ubelgiji akiwa na mabao 25 na kuisaidia Genk kutwaa taji huku akiiwezesha kucheza Champions League. Mbali na hayo Samatta, alitwaa tuzo ya Ebony Shoe akizawadiwa kama mchezaji bora kutoka Afrika. Mshambuliaji huyo wa Taifa Stars amehusishwa pia kutaka kusajiliwa na klabu nyingi za England ambazo zinashiriki Premier League zikiwemo Leicester, Aston Villa na Watford.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako