• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Afrika zaingia kwenye mwongo mpya wa uhusiano wenye nguvu kupitia ushirikiano wenye manufaa

    (GMT+08:00) 2020-01-07 16:19:44

    Mjumbe wa Taifa wa China ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Bw. Wang Yi leo anaanza ziara ya siku 7 barani Afrika, ikiwa ni ziara yake ya kwanza kwa nchi za nje kwa mwaka 2020. Ziara hii inaashiria miaka 30 mfululizo ambapo waziri wa mambo ya nje wa China ametembelea nchi za Afrika mwanzoni mwa kila mwaka kuanzia mwaka 1991.

    Utamaduni mzuri ambao umedumishwa kwa muda mrefu tayari unazungumzia mengi kuhusu asili ya uhusiano wa kindugu na unaoshamiri kati ya China na Afrika, na mwaka huu wa 2020 una umuhimu mkubwa kwa pande zote mbili kwa kuwa pande hizo zinaingia kwenye uhusiano wenye nguvu zaidi unaodumishwa na utamaduni na ushirikiano wa kunufaishana.

    Utamaduni wa Waziri wa Mambo ya Nje wa China kutembelea Afrika mwanzoni mwa kila mwaka ulianza Januari mwaka 1991 wakati aliyekuwa naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa China Qian Qichen alipotembelea nchi nne za Afrika. Umekuwa ni mwelekeo usioweza kuachwa baada ya warithi wake, wakiwemo Tang Jiaxuan, Yang Jiechi na Wang Yi kuendelea kuchagua Afrika kwa ziara zao za kwanza za mwanzo wa mwaka. Lengo hasa ya utamaduni huo, kama hayati Qian alivyouita, ni kwa sababu China inaamini kuwa nchi nyingi duniani zilikuwa zinaanza kutegemeana sana, hususan tangu mwisho wa Vita ya Baridi, na Afrika, kama kundi kubwa la nchi katika familia ya Umoja wa Mataifa, inawakilisha nguvu muhimu katika masuala ya kimataifa. Akasema kuanzisha ushirikiano wa kirafiki na Afrika, kunasaidia kutimiza maslahi ya China. Zaidi ya hayo, China, ikiwa ni nchi kubwa inayoendelea duniani, inapaswa kuimarisha mshikamano na ushirikiano na Afrika na nchi nyingine za dunia ya tatu kwa sababu hiyo ndio nguzo kuu ya sera ya mambo ya nje ya China.

    Mwaka huu pia ni maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, (FOCAC) ambalo linalenga kuboresha ushirikiano kati ya pande hizo mbili na kupanua maafikiano katika masuala yanayofuatiliwa na pande hizo mbili. Tangu kuanzishwa kwa FOCAC mwaka 2000, China na Afrika zimeshuhudia matokeo yasiyotazamiwa ya ushirikiano. China imekuwa mwenzi mkubwa wa biashara wa Afrika kwa miaka 10 mfululizo, na mwaka 2018, thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 204, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 ikilinganishwa na mwaka 2017. Kwa upande wa miundombinu, uzoefu na teknolojia ya China umekuwa na manufaa makubwa katika mirafi mikubwa ya miundombinu kama vile njia za reli, bandari, viwanja vya ndege na vituo vya kuzalisha umeme barani Afrika. Katika mkutano wa FOCAC uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini mwaka 2015, China ilitangaza mipango 10 ya ushirikiano ili kuboresha mageuzi ya kiviwanda na kilimo cha kisasa barani Afrika, pamoja na kutoa fedha kiasi cha dola za kimarekani bilioni 60. Wakati wa kufungua mkutano wa FOCAC wa mwaka 2018 uliofanyika hapa Beijing, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuongeza dola bilioni 60 zaidi za ufadhili barani Afrika.

    Mwaka uliopita umeshuhudia Afrika ikizindua awamu ya utendaji wa Eneo la Biashara Huria Barani Afrika (AfCFTA), na kuunda kile kinachoweza kuwa eneo kubwa zaidi la biashara huria duniani, lenye watu zaidi ya bilioni 1.2, likiwa na pato la ndani la dola za kimarekani trilioni 2.5.

    Kamishna wa Biashara na Viwanda wa Umoja wa Afrika Bw. Albert Muchanga amesema, kutokana na kuanza utekelezaji wa Eneo hilo, pendekezo la China la Ukanda Mmoja na Njia Moja linatoa fursa kubwa zaidi kwa Afrika kuendeleza miradi yake mikubwa ya miundombinu na kujenga mtandao wa usafirishaji unaounganisha sehemu mbalimbali za bara hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako