• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Utafiti waonyesha kuwa nyongeza ya ushuru inayotozwa na Marekani inalipwa na kampuni na watu wa nchi hiyo

  (GMT+08:00) 2020-01-07 16:21:50

  Nyongeza ya ushuru inayotozwa na serikali ya Marekani dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi hiyo inalipwa kwa kiasi kikubwa zaidi na kampuni na wateja wa Marekani, na kwamba mpango mpya wa biashara wa kujibu ushuru huo umepangwa kwa kasi.

  Hayo yamo kwenye ripoti iliyotolewa jana na Mamlaka ya Taifa ya Utafiti wa Uchumi ya Marekani, na ni sawa na matokeo ya tafiti nyingi zilizofanywa awali.

  Utafiti huo uliofanywa kwa pamoja na mtafiti wa Benki ya New York Mary Amiti, profesa Stephen Redding wa Chuo Kikuu cha Princeton na profesa David Weinstein wa Chuo Kikuu cha Columbia, pia umegundua kuwa mpango mpya wa mlolongo wa utoaji bidhaa umefanywa kwa kasi ili kuendana na nyongeza ya ushuru dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako