• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalam wa Uingereza asema miaka 10 ijayo itaendelea kuwa ya China

    (GMT+08:00) 2020-01-07 17:09:02

    Gazeti la The Guardian la Uingereza limetoa makala ya mtaalam wa Chuo Kikuu cha Cambridge Bw. Martin Jacques na kusema, miaka 10 iliyopita ilikuwa ni miaka ya China, na miaka 10 ijayo pia ni itakuwa ya China.

    Makala hiyo imesema, katika kila mwaka wa miaka 10 iliyopita, chanzo kikuu cha ukuaji wa uchumi wa dunia kilikuwa China, sio Marekani. Mwaka 2014, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Benki ya Dunia, China iliipiku Marekani na kuwa nchi yenye uchumi mkubwa zaidi duniani, ikihesabiwa kwa kiwango cha usawa cha sarafu tofauti, na hivi sasa, uchumi wa China umekuwa mara mbili ikilinganishwa na mwaka 2010.

    Makala hiyo pia imesema, kama inavyotarajiwa, nchi za magharibi hazitaki kukubali hali hiyo halisi. Kuibuka kwa China kumekuwa tishio kwa Marekani na Ulaya, tishio ambalo litaendelea katika karne hii. Nchi za magharibi zilidhani kuwa China inajua kuiga tu, lakini China imethibitisha uwezo wake wa kuvumbua. Mkoa wa Shenzhen, nchini China unaweza kushindana na eneo la Silicon Valley la nchini Marekani. Makampuni ya Huawei, Tencent na Alibaba ya China pia yanaweza kusimama pamoja na makampuni ya Microsoft, Google, Facebook na Amazon ya Marekani. Mwaka 2018, idadi ya hataza zilizoombwa na China imechukua asilimia karibu 50 duniani.

    Makala hiyo pia imesema, pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja ambalo nchi zaidi ya 100 zinashiriki ni ishara ya ongezeko la ushawishi wa China. Pia linatarajia kutambuliwa kuwa mfumo wa utaratibu mpya wa dunia ambao unazingatia zaidi masuala ya maendeleo yanayofuatiliwa zaidi na nchi zinazoendelea.

    Katika miaka 10 ijayo, mfumo wa kimataifa unaozunguka nchi za magharibi utaendelea kusambaratika, na ushawishi wa China kwa mfumo huo utaongezeka, mchakato ambao hautazuiliwa..

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako