• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Gor, Tusker wajikita kileleni Homeboyz, Ulinzi wakipaa

  (GMT+08:00) 2020-01-07 17:38:34

  Kakamega Homeboyz, Ulinzi Stars na Kariobangi Sharks zimepiga hatua moja mbele kila mmoja baada ya kuzoa alama muhimu katika mechi za kufungua mwaka wa 2020 wikendi. Mabingwa watetezi Gor Mahia na washindi wa zamani Tusker wanasalia katika nafasi mbili za kwanza kwa alama 32 na 31. Viongozi Gor walibwaga Wazito 1-0 nao wanamvinyo wa Tusker wakaandikisha ushindi mkubwa msimu huu wa mabao 7-0 dhidi ya Chemelil Sugar. Homeboyz, ambayo itachuana na Gor Januari 12, imepaa nafasi moja hadi nambari tatu baada ya kuilipua Kisumu All Stars 4-0. Uhasama kati ya Gor na Homeboyz ulianzishwa na mmiliki wa Homeboyz, Cleophas 'Toto' Shimanyula alipojipiga kifua kabla ya mechi ya mkondo wa kwanza mwezi Novemba kuwa timu yake itakanyaga vijana wa Steven Polack kabla ya kulimwa 3-0.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako