• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Chelsea yafuzu baada ya kunyanyasa Forest

  (GMT+08:00) 2020-01-07 17:38:51

  Mabao mawili dhidi ya Nottingham Forest katika kipindi cha kwanza kutoka kwa Callum Hudson-Odoi na Ross Barkley, Jumapili usiku yalitosha kuipa Chelsea ushindi wa kusonga mbele katika michuano ya kuwania ubingwa wa FA Cup. Mbali na kufunga bao la kwanza, kinda Odoi kadhalika alichangia katika kupatikana kwa bao la pili. Kulikuwa na utata katika mechi hiyo, na ilibidi mtambo wa VAR utumike kumsaidia mwamuzi ambaye alikuwa amewapa Forest penalti kwa madai kwamba mshambuliaji Alexander Mighton alikuwa ameangushwa na Fikayo Timori katika eneo la hatari, uamuzi ambao ulikataliwa na mtambo huo ulioonyesha kwamba kabla ya kitendo hicho, mchezaji wa Forest alikuwa ameotea. Mechi hiyo ilikuwa ya kihistoria kwa klabu ya Chelsea ambayo inasherehekea miaka 50 tangu inyakue ubingwa wa taji hilo kwa mara ya kwanza 1970 chini ya Dave Sexton.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako