• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Iran yaiweka wizara ya ulinzi ya Marekani kwenye orodha ya kundi la kigaidi

  (GMT+08:00) 2020-01-07 17:49:01
  Shirika la habari la Iran limesema, bunge la nchi hiyo leo limeitaja wizara ya ulinzi ya Marekani kuwa ni kundi la kigaidi.

  Habari zinasema, kwa mujibu wa kura zilizopigwa na wabunge wa Iran, idara zote na kampuni zenye ushirika na wizara ya ulinzi ya Marekani, na makamanda wa Marekani waliopanga na kumwua aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC Bw. Qassem Soleimani, wamewekwa kwenye orodha ya kundi la kigaidi.

  Wakati huohuo, Televisheni ya Iran imeripoti kuwa watu zaidi ya 35 wameuawa na wengine 48 kujeruhiwa kwenye tukio la kukanyagana katika mazishi ya jenerali Soleimani iliyofanyika mjini Kerman, nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako