• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Microsoft yamteua Kendi Ntwiga kama Msimamizi wa oparesheni zake Kenya

  (GMT+08:00) 2020-01-07 19:11:24
  Kampuni ya Microsoft imemteua Kendi Ntwiga - Nderitu kama Msimamizi wa oparesheni zake nchini Kenya.

  Taarifa kutoka Microsoft ilimtaja Kendi kama mtu mwenye nidhamu, kiongozi wa biashara na uzoefu zaidi ya miaka 15 katika tasnia ya habari na mawasiliano.

  Amesema amefurahi kujiunga na Microsoft wakati wa huu Afrika ikikuza maendeleo ya dijitali.

  Katika jukumu lake jipya, atakuwa na jukumu la kukuza na kudumisha uhusiano kwa kampuni zote na idara za uuzaji.

  Kabla ya kujiunga na Microsoft, Bi Nderitu aliwahi kuwa Meneja Mkuu wa Afrika Mashariki, Magharibi na Kati katika kampuni ya Check Point Software.

  Aidha amewahi kufanya kazi na huko Oracle, HP na Intel, akiwa na jukumu la kuongoza na kutekeleza mikakati ya biashara eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako