• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Oparesheni zakua bandari ya Mombasa

  (GMT+08:00) 2020-01-07 19:11:39

  Bandari ya Mombasa nchini Kenya imepata ukuaji kutokana na ujenzi wa Kituo cha pili cha kupakua shehena, kuboreshwa kwa huduma za upakuaji na uchukuzi wa haraka wa mizigo kupitia kwa reli ya SGR kwenda Nairobi.

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari ya Kenya, Daniel Manduku alisema msongamano wa umepunguza na kuwezesha shughuli kufanyika kwa haraka.

  Alisema bandari hiyo ilishughulikia kakontena milioni 1.425 mnamo 2019 ikiwakilisha ukuaji wa asilimia 7.3 zaidi ya mwaka uliopita.

  Bwana Manduku alisema usafirishaji wa haraka wa shehena kwa njia ya Reli kwenda kwa bandari kavu mjini Nairobi umetatua msongamano wa bandari na sasa wanatarajia kupeleka treni zaidi ya 10 kila siku.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako