• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Waziri wa fedha awataka wafanyabishara kulipa kodi

    (GMT+08:00) 2020-01-07 19:12:14
    Waziri wa Fedha wa Uganda Matia Kasaija amesema serikali inaweza kutoa huduma tu ikiwa watu wanalipa ushuru.

    Akiongea wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Jumuiya ya Ujasiriamali Ulimwenguni jijini Kampala, Bwana Kasaija, alisema wajasiriamali lazima waheshimu majukumu yao ya ushuru ili kuwezesha serikali kuendeleza miundombinu na huduma zinazosaidia maendeleo ya biashara.

    Alisema utendaji wa mapato ya ushuru bado uko chini sana na hauwezi kusaidia mahitaji ya maendeleo ya nchi kwa sababu baadhi ya wafanyabishara hawalipi ushuru.

    Kulingana na Uchunguzi Ujasiriamali na Uchumi wa Wajasiriamali, biashara nyingi nchini Uganda zinachagua ukuaji mdogo ili kuzuia kulipa kodi.

    Ili kuwezesha upatikanaji wa mtaji kwa biashara ndogo ndogo, Bwana Kasaija alisema, serikali itatenga Shilingi bilioni 100 katika mwaka wa fedha 2020/21 ili kuwezesha wajasiriamali wadogo kupata mkopo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako