• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tazania: Vijana kwenye sekta za uvuvi na mifugo kunufaika

  (GMT+08:00) 2020-01-07 19:12:43
  Vijana kutoka mikoa 13 ya Tanzania Bara na Visiwani watanufaika na mtandao wa vijana unaojihusisha na shughuli za uvuvi na mifugo.

  Lengo la kuanzishwa kwa mtandao huo kutawasaidia vijana nchini, kujiajiri moja kwa moja kupitia mtandao huo wa uvuvi na mifugo.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtandao huo, uliofanyika jijini Arusha, Rais wa Mtandao huo, Laban Boaz, alisema vijana chini ya miaka 35, kutoka mikoa hiyo, watanufaika na mtandao huo kwa kufundishwa mbinu bora za kisasa za ufugaji.

  Alisema lengo la kuanzishwa kwa mtandao huo, ni kuhamasisha vijana nchini, kujiajiri katika sekta ya mifugo na uvuvi kwa kutumia njia ya kisasa ambazo zitasaidia kuongeza uzalishaji mali na ajira kwa vijana.

  Alisema walianzisha mtandao huo, baada ya kuona kuna mwanya wa kimaendeleo kati ya wazee na vijana.

  Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Felix Nandonde, alisema mtandao huo ni juhudi za muda mrefu zilizofanywa na Umoja wa Afrika kupitia mradi wa kuendeleza rasilimali za wanyama (AU-IBAR).

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako