• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Putin wa Russia afanya ziara nchini Syria

  (GMT+08:00) 2020-01-08 08:42:59

  Rais Vladimir Putin wa Russia amewasili Damascus, ambako amefanya mazungumzo na mwenzake wa Syria Bashar al-Assad. Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Putin kufanya ziara nchini Syria tangu mgogoro wa Syria uzuke mwaka 2011.

  Habari kutoka televisheni ya Syria zinasema Marais Putin na Al-Assad wamefanya mazungumzo kwenye kambi ya jeshi la Russia iliyoko mjini Damascus, ambako wamesikiliza ripoti iliyotolewa na kamanda wa jeshi la Russia nchini Syria, na kujadili hali ya Syria na ya kikanda, ikiwa ni pamoja na hali ya eneo la Idlib na kaskazini mwa Syria, masuala juu ya kupambana na ugaidi na kuhimiza mchakato wa kisiasa nchini Syria.

  Rais al-Assad amelishukuru jeshi la Russia kwa juhudi zake za kushirikiana na jeshi la Syria katika kupambana na waasi wenye itikadi kali nchini Syria tangu mwezi Septemba mwaka 2015.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako