• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sadio Mane atwaa tuzo za CAF na kuwashinda MO Salah na Riyad Mahrez

  (GMT+08:00) 2020-01-08 09:11:54

  Usiku wa tuzo za CAF ziolizotolewa nchini Misri katika jiji la Cairo umemalizika kwa kushuhudia watu mbalimbali wakishinda tuzo. Sadio Mane wa Liverpool na timu ya taifa ya Senegal ndio aliibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika mwaka 2019 kwa kuwashinda MO Salah wa Liverpool na Riyad Mahrez wa Man City. Golikipa wa zamani wa Togo Kodjovi Obilale aliyepewa tuzo maalum, alistaafu soka 2010 akiwa na miaka 26 kufuatia kushambuliwa kwa bus la Togo nchini Angola na kupata ulemavu wa maisha, katika ajali hiyo alikuwa Adebayor na Vincent Bossou aliyewahi kucheza Yanga. Achraf Hakim wa Real Madrid aliyepo kwa mkopo Borussia Dortmund yeye amekuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora kijana 2019. Kwa upande wa timu bora za taifa, timu ya taifa ya wanawake ya Cameroon imenyakua tuzo ya timu bora ya taifa ya wanawake 2019 na timu ya wanaume ya taifa ya Algeria ikajishindia tuzo ya timu bora ya taifa ya mwaka 2019, Algeria ndio waliibuka Mabingwa wa AFCON 2019. Kocha wa Algeria aliyeipa Ubingwa wa AFCON 2019 nchini Misri Djamel Belmadi ametangazwa kocha bora wa Afrika kwa mwaka 2019.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako