• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Saimon Msuva wa Tanzania kutimkia timu ya Benfica ya ligi kuu nchini Ureno

  (GMT+08:00) 2020-01-08 09:12:14

  Mshambuliaji wa Tanzania na klabu ya Difaa El-Jadidi ya nchini Morocco, Saimon Msuva amesaini Mkataba wa miaka mitatu kuitumikia timu ya Benfica inayoshiriki ligi kuu nchini Ureno. Licha ya mkataba huo nyota huyo wa Taifa Stars atapelekwa kwa mkopo wa miezi sita katika klabu ya Panathiakos ya Ugiriki. Msuva anatarajiwa kuondoka Difaa Januari 15, 2020 kwenda Ureno kisha kutimkia Ugiriki ambapo atarejea kwa waajiri wake hao wapya Julai 2020. Inadaiwa Yanga haitapata Mgao wowote kwa usajili huo wa Simano Msuva baada ya kukataa kipengele cha mgao kama atauzwa nje ya Difaa El Jadid na kutaka kulipwa Dola 100, 000 badala ya Dola 80, 000 ambayo Difaa walikusudia kuitoa kama kipengele hicho kingekuwepo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako