• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Malkia Strikers wako ukingoni kuinyakua tiketi ya Olimpiki ya Tokyo 2020

  (GMT+08:00) 2020-01-08 09:12:33

  Timu ya taifa ya Kenya ya volleyball kwa upande wa wanawake Malkia Strikers jana ilikuwa ikimenyana na wenyeji wao Cameroon kwenye michuano ya Afrika ya kufuzu michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 inayoendelea katika uwanja wa ndani wa Palais polyvalent des sports (Paposy). Vipusa hao wa Kenya wamewaonesha mahasimu wao kwamba wamekwenda kwa kazi moja tu ya kunyakua ushindi baada ya kuigaragaza Cameroon kwa 3-2. Baada ya Kenya kupata ushindi mashabiki wenyeji waliokuwa wakishangilia usiku kucha walianza kuchomoka mmoja baada ya mwingine wakijua kuwa tiketi ya olimpiki imewaponyoka. Ushindi huo umeifanya Malkia Strikers kuwa na point nane na ushindi dhidi ya Nigeria utawashuhudia mabingwa hao mara nane wa Afrika wakirejea tena kwenye michezo ya Olimpiki baada ya miaka 16 bila ya kujali matokeo kati ya Misri na Cameroon zitakazovaana leo. Cameroon ina pointi saba na inaweza kufuzu kama Kenya kesho itashindwa na Nigeria ambayo inashika mkia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako