Manchester City imepata kulipiza kisasi kwa kuwapa funzo mahasimu wao Manchester United baada ya kuwaonjesha machungu ya kufungwa walipopachika 3-1 kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Carabao Cup uliochezwa jana Old Trafford. United waliwashinda City 2-1 walipokutana mara ya mwisho kwenye Premier League Disemba 7, lakini kuwashinda tena ilikuwa ngumu baada ya kikosi cha Pep Guardiola kuonekana kuimarika na kuwakamata barabara mahasimu wao. Bernardo Silva alifungua njia ya magoli kwa wageni hao baada ya kurusha shuti kali kutoka umbali wa yadi 20 katika dakika ya 17 ambalo liliingia kimiani kabla ya David De Gea kupata muda wa kulifukuzia. Magoli mengine ya Manchester City yalifungwa na Riyad Mahrez na Andreas Pereira. Nao United bao la kujitoa kimasomaso liliingizwa wavuni na Rashford katika dakika ya 70.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |