• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wateleza kwenye barafu wa Kenya wapelekwa Korea Kusini kujiandaa na Olimpiki ya baridi ya Beijing

    (GMT+08:00) 2020-01-08 09:13:08

    Kenya imewapeleka Korea Kusini wachezaji wake wa kuteleza kwenye barafu kwa ajili ya mafunzo ikiwa inaongeza mipango yake ya kuingiza angalau wanariadha watano katika Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing 2022. Mwaka 2018, Sabrina Wanjiku Simader alikuwa mchezaji pekee kwenye mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika PyeongChang, Korea Kusini. Mtelezaji huyo anayeishi Vienna ameshindana kwenye mashindano mawili ya kuteleza kwenye barafu. Katibu mkuu wa Kamati ya Taifa ya Olimpiki ya Kenya Francis Mutuku amesema wamewashawashi wanamichezo wengi kujiunga na mashindano ya olimpiki ya baridi licha ya kwamba nchi hiyo haina theluji. Wachezaji waliokwenda Korea Kusini ni pamoja na Chebet Njeri Koech, Chumbana Likiza Muhusini na Hassneni Ali Shah ambao watajumuika na kocha wao wa viatu vya magurudumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako