• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM waunga mkono utulivu wa Iraq na kuhimiza kujizuia katika kukabiliana na mgogoro

    (GMT+08:00) 2020-01-08 09:34:06

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais Barham Salih wa Iraq na kusisitiza kuwa Umoja wa Mataifa unaunga mkono utulivu wa Iraq na kuhimiza kujizuia ili kukabiliana na mgogoro.

    Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Bw. Salih inasema kwenye mazungumzo yao, pande mbili zimejadili hadhi ya jumuiya ya kimataifa katika hali mpya ya kikanda na kimataifa.

    Taarifa hiyo pia imesema Umoja huo umeeleza wasiwasi kubwa kuhusu kupamba moto kwa matishio yanayokabili amani na usalama wa kimataifa, huku ikisisitiza haja ya kujizuia na kutumia busara wakati wa kukabiliana na mgogoro.

    Habari nyingine zinasema, jeshi la Ujerumani limesema kutokana na kusimamishwa kwa operesheni za mafunzo zilizofanywa nchini Iraq na kuzingatia hali ya usalama ya hivi sasa, askari 35 wa nchi hiyo walioko mjini Baghdad na maeneo mengine wamehamishwa nchini Kuwait na Jordan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako