Televisheni ya Iran imemnukuu mkuu wa Huduma ya Matibabu ya Dharura ya nchi hiyo Bw. Pierre Hussein Culiwand na kusema kuwa tukio la kukanyagana lililotokea katika mazishi ya kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Qassem Soleimani, limesababisha vifo vya watu 56 na wengine 213 kujeruhiwa.
Video ya televisheni imeonyesha kuwa baadhi ya watu wakilala chini mitaani, wengine wakiomba msaada, na madaktari wa dharura wakiwapatia wagonjwa matibabu ya papo kwa hapo. Tukio hilo lilichelewesha kwa muda wa mazishi ya Soleimani, na Rais Hassan Rouhani wa Iran ametoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |