• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Seneti la Marekani lina kura za kutosha kuanza mchakato wa kufungua kesi dhidi ya rais wa nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2020-01-08 16:02:47

    Kiongozi wa wabunge wengi katika Baraza la Seneti nchini Marekani Mitch McConnell amesema, amepata kura za kutosha kwa ajili ya bunge la juu la nchi hiyo kufungua kesi dhidi ya rais Donald Trump.

    Kesi hiyo bado haijaanza kutokana na wabunge wa vyama vya Democrats na Republican kuendelea kuvutana juu ya kanuni zake.

    Mwezi uliopita, Rais Trump alifunguliwa mashtaka na bunge lenye wabunge wengi wa chama cha Democrats kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka yake na kuzuia bunge kutimiza majukumu yake. Lakini kanuni za kumfungulia mashtaka hazijafikishwa kwenye baraza la Seneti, ambapo wabunge wa Republican ni wachache.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako