• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: KMKM yaja juu beki wao kutajwa Singida United

  (GMT+08:00) 2020-01-08 16:49:44

  Benchi la ufundi la Kikosi cha Kuzuia Magendo Zanzibar, (KMKM), limekanusha tetesi ambazo zinaendelea kuvuma, baada kudaiwa mchezaji wao Haji Mwinyi Ngwali amejiunga na timu ya Singida United ya Tanzania bara. Kocha mkuu wa timu hiyo Ame Msim Khamis amesema uongozi hauna taarifa yoyote juu ya habari hizo, kwani mchezaji huyo anaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi zilizobaki za ligi kuu Zanzibar. Alisema hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliofanywa juu ya mchezaji huyo. Kwa upande wake, mchezaji huyo alisema anachofahamu kuwa ni mchezaji wa timu ya KMKM kutokana ndio anayoendelea kuitumikia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako