• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyakazi 2,000 mradi wa Lapsset watumwa nyumbani, waambiwa wasubiri neno la mwajiri

    (GMT+08:00) 2020-01-08 18:27:39

    Wafanyakazi zaidi ya 2,000 wanaoendeleza ujenzi wa mradi wa Bandari Mpya ya Lamu (Lapsset) wametumwa nyumbani ghafla baada ya mkandarasi wa mradi huo kuhofia huenda wafanyakazi hao wakalengwa na kushambuliwa na wapiganaji wa al-Shabaab.

    Hii ni kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa al-Shabaab mapema wiki hii katika eneo la Manda-Magogoni, Kaunti ya Lamu.

    Eneo la Kililana ambako Lapsset inajengwa ni umbali wa kilomita moja pekee kutoka kambi ya wanajeshi wa Marekani iliyoshambuliwa ya Manda-Magogoni.

    Kampuni iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa Lapsset ya China Communications Construction Company (CCCC), imewafahamisha wafanyakazi wake wote kwamba shughuli za ujenzi eneo hilo zimesitishwa kwa muda na kwamba vibarua wote wanatakiwa kurudi nyumbani.

    Meneja wa Lapsset, tawi la Lamu, Salim Bunu, amesema tayari wameanzisha mazungumzo na mwanakadnarasi ili shughuli zirejelewe hivi karibuni.

    Afisa wa Halmashauri ya Bandari (KPA), tawi la Lamu, Abdishukri Osman pia amethibitisha kufungwa kwa shughuli za ujenzi eneo la Lapsset.

    Bw Osman alisema majadiliano yanaendelea kati ya mwanakandarasi, KPA, idara ya usalama na Lapsset kwa jumla ili kuona kwamba shughuli zinarejelewa mara moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako