• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Riba kubwa mikopo zamkwaza Mpango

  (GMT+08:00) 2020-01-08 18:27:55
  Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Bw Philip Mpango amewaonya watendaji wa serikali dhidi ya kutoza riba kubwa ambazo zinawaumiza wananchi.

  Amewataka watumishi wa umma ambao wanaendesha maeneo ya huduma ndogo za fedha kuacha mara moja kabla serikali haijawabaini na kuwachukulia hatua kali.

  Dk. Mpango alisema kuwa moja ya changamoto nchini humo katika uendeshaji wa huduma ndogo za fedha ni riba kubwa za mikopo ambazo zimekuwa zikitolewa katika maeneo mbalimbali ya nchi.

  Alisema hivi sasa watoa huduma ndogo za fedha, wamekuwa na tabia ya kujipangia riba vile wanavyotaka ili kujipatia faida kwa haraka bila kujali wananchi wanaowakopesha.

  Dk. Mpango alimwagiza Gavana wa Benki Kuu (BOT) kuhakikisha kuwa anaitisha mkutano wa nchi nzima utakaowajumuisha watoa huduma wote wa huduma ndogo za fedha.

  Kuhusu changamoto ya utengenezaji na usambazaji wa fedha bandia, Dk. Mpango alisema hilo ni jambao ambalo linamuumiza sana kwa kuwa linaathiri uchumi wa nchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako