• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • DRC kupambana na umaskini

  (GMT+08:00) 2020-01-08 18:28:11

  Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesisitiza nia yake ya kuhakikisha kuwa inapambana na umaskini ambao umekithiri nchini humo.

  Serikali ya rais Tshisekedi imesema inalenga kuwaondoa raia milioni 20 wa nchi hiyo kutoka kwenye umaskini uliokithiri katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Idadi hiyo ni robo ya wakaazi wanaokadiriwa nchini DRC. Awali rais Tshisekedi alikuwa ametoa ahadi hiyo baada ya kufanyika kwa utafiti kuhusu umaskini nchini humo. Utafiti huo ulifanywa kwa kuzingatia kupindi cha kati ya mwaka 2005 na 2012. Kuna kipindi kifupi ambapo umasikini ulipungua kwa alama nane na kufikia karibu asilimia 63.4. Tangu wakati huo, takwimu zinaonyesha kuwa hali haijabadilika sana. Mwaka 2017, kiwango cha umasikini kilikadiriwa kuwa asilimia 63, na hata 70% vijijini. Miongoni mwa mambo ambayo serikali ya Tsetekedi inapania kufanya ni kuboresha miundombinu nchini humo na huduma za kijamii na kiuchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako