• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SIDO yatengeneza mashine 273

  (GMT+08:00) 2020-01-08 18:28:26

  Shirika la viwanda Vidogo (Sido) mkoani Mbeya nchini Tanzania kupitia Kituo cha Uendelezaji wa Teknolojia, limefanikiwa kutengeneza mashine 273 kwa ajili ya wajasiriamali wadogo ikiwa lengo ni kuanzisha viwanda vidogo nchini humo.

  Msimamizi wa karakana Sido mkoani humo, Japhet Kasonda, amesema mashine hizo ni kwa ajili ya kusaidia kuchakata mazao yanayolimwa Mbeya na mikoa jirani ya Iringa, Rukwa, Njombe na Songwe.

  Alisema zaidi ya ajira 700 zimeweza kupatikana kutokana na utengenezaji wa mashine hizo katika maeneo tofauti ya mkoa wa Mbeya, ambapo wananchi wengi wamezinunua na kuanzisha viwanda vidogo ambavyo vimewasaidia kujipatia ajira.

  Kasonda alisema kuwa miongoni mwa mashine zinazotengenezwa na kituo hicho hadi sasa ni za kuchakata mahindi zikiwamo mashine za kupukuchua mahindi, mashine za kukoboa mahindi, mashine kubwa na ndogo za kusaga unga pamoja na mitambo ya kisasa kwa ajili ya kusaga unga.

  Alizitaja mashine zingeni kuwa ni za kuchakata alizeti zikiwamo mashine za kukamua mafuta, mashine za kuchuja mafuta, mashine za kuchekecha alizeti na utengenezaji wa matangi ya kisasa ya kuhifadhia mafuta ya alizeti.

  Alisema uamuzi wa wajasiriamali katika kuanzisha viwanda vidogo kutaongeza thamani ya mazao pamoja na kuchangamkia fursa za kibiashara ndani ya nchi na katika nchi jirani kutokana na kuzalisha bidhaa zenye ubora kutokana na mchango wa ubunifu na utengenezaji wa mashine za kisasa zinazofanywa na kituo cha kuendeleza teknolojia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako