• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na katibu mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu

    (GMT+08:00) 2020-01-08 18:52:34

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi yuko ziarani nchini Misri, na amekutana na katibu mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu Bw. Aboul Gheit.

    Katika mkutano wao, Bw. Wang amesema, China ni mwenzi wa kuaminika wa Umoja huo, na pande hizo mbili zinatakiwa kuendelea kuimarisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati, kuungana mkono, kulinda amani na haki ya kimataifa na kuhimiza utatuzi wa kisiasa wa masuala yanayofuatilia zaidi ya kikanda. Pia amesema China inazingatia nafasi ya Umoja huo na kusifu msimamo wake wenye haki katika masuala muhimu ya kimataifa na ya kikanda. Amesema China itaendelea kuunga mkono nchi za kiarabu zikabiliane na matatizo na changamoto zilizopo chini ya uratibu wa Umoja huo.

    Bw. Wang pia amesema, China inashukuru uungaji mkono wa Umoja huo katika suala la Xinjiang, na inawakaribisha maofisa wa Umoja huo kutembelea mkoa wa Xinjiang kuangalia mafanikio yaliyopatikana katika kupambana na ugaidi na kuthibitisha uhuru wa kidini, utulivu na ustawi wa mkoa huo.

    Kwa upande wake, Bw. Gheit amesema, Umoja huo unatilia maanani kuendeleza uhusiano wake na China, na kwamba nchi wanachama wa Umoja huo zinapenda kujadiliana na China kuhusu kujenga jumuiya ya pande hizo mbili yenye hatma ya pamoja.

    Bw. Gheit ameongeza kuwa, Umoja huo unaunga mkono msimamo wa China katika suala la Xinjiang na kupinga uingiliaji wa nje wa mambo ya ndani ya China. Pia unasaifu msimamo wenye haki wa China na mchango wake katika masuala yanayofuatilia zaidi ya Mashariki ya Kati. Ameishukuru China kwa kuunga mkono watu wa kiarabu hasa watu wa Palestina kupigania haki yao halali.

    Habari zinasema, Misri ni kituo cha kwanza cha ziara ya waziri wa mambo ya nje wa China katika nchi tano za Afrika. Baadaye, Bw. Wang pia atatembelea Djibouti, Eritrea, Burundi na Zimbabwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako